Isaiah 13:15-18


15 aYeyote atakayetekwa atapasuliwa tumbo,
wote watakaokamatwa watauawa kwa upanga.

16 bWatoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande
mbele ya macho yao;
nyumba zao zitatekwa
na wake zao watatendwa jeuri.


17 cTazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao,
ambao hawajali fedha
wala hawafurahii dhahabu.

18 dMishale yao itawaangusha vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga
wala hawataangalia watoto kwa huruma.
Copyright information for SwhKC